Sambaza

Wema Afungukia Ukimya Wake, Atambulisha ‘Wema Empire’

Muigizaji ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, baada  ya kuwa kimya kwa kipindi leo Julai 26, 2019 amefika katika ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori jijini Dar na kuanika sababu za ukimya wake huku akitambulisha kampuni yake mpya ya ‘Wema Sepetu Empire’.

Akizungumza mapema leo ndani ya +255 Global Radio, Wema aliyekuwa ameongozana na Director wake, Neema Ndepanya, alisema kuwa ukimya wake ulikuwa ni sababu ya kujipanga kuja na tamthiliya kubwa ambayo itakuwa chini ya Wema Sepetu Empire.

Mahojiano yakiendelea.

“Wema Sepetu Empire ni kampuni ambayo ipo chini ya Endless Fame inayosimamia filamu zangu kwa muda mrefu. Siku zote naamini katika kula na wenzangu mimi siyo mchoyo hata marehemu Kanumba (Steven) aliniona na kunipa hii nafasi, kwa nini nisimpe mtu mwingine? Mimi ni mwanadamu halafu ni mwanadamu mzuri, tatizo watu tu!

“Mtaani kuna wasanii wachanga wengi hawajui wanaanzia wapi wanaenda wapi? Nilikuwa napokea simu hata 200 hadi 300 kwa siku moja kutoka kwa hawa wasanii wachanga wakiniomba niwasaidie.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey