Kesi Ya A$AP Rocky Yamvuruga Akili Trump
Rapa A$AP Rocky bado anaendelea kusota jela kwa mashtaka ya kumpiga shabiki na kumjerui nchini Sweden kwa kesi hiyo huwenda akahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Rais Donald Trump ameguswa na taarifa hizo hivyo kumjia juu Waziri Mkuu wa Sweden. kupitia ukurasa wake wa twitter alitweet
“Nimevunjika sana moyo na matendo ya Waziri Mkuu Stefan Löfven, Sweden imewaangusha wa Marekani Weusi wote nchini Marekani. Nimeutazama mkanda wa ASAP Rocky, na nimeona alikuwa akifuatwa na kusumbuliwa na watu ambao walikuwa wanatafuta matatizo. Hebu tuwatendee haki Wamarekani.” Ameandika Trump na kumalizia kwa Hashtag ya #FreeRocky
Toa Maoni Yako Hapa