Sambaza

Zari Acharuka Ukumbini baada ya Kuitwa ‘Mama’, Azomewa

Zarithebosslady, ambaye ni mzazi mwenza wa Msanii Diamond Platnumz alikuwa ni mmoja kati ya majaji katika shindano la Miss Uganda lililofanyika Weekend Iliyopita, siku ya Jumamosi tarehe 27 July, 2019. 

Katika hali isiyotarajiwa, Zari aliingia kwenye vita ya maneno na Anita Fabiola ambaye ndiye alikuwa ‘Host ‘ ya show hiyo baada ya Anita kumtaka Zari asome majina ya warembo walioingia ‘Top three’. Zari alipatwa na hasira baada ya kuitwa ‘Mama’ na Anita mbele ya watu kitendo kilichomfanya Zari ashikwe na hasira na kugoma kusoma majina hayo. Kitendo hicho kiliwakera watazamaji na kuamua kumzomea Zari hali iliyofanya ukumbi mzima kujawa na taharuki.

Mpaka sasa Zari hajazungumza chochote kuhusiana na tukio hilo lakini mashabiki wengi mitandaoni wamekuwa wakimshambulia kwa maneno makali kutokana na kitendo hicho cha kuanzisha ‘varangati’ kwa sababu ndogo kama ile.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey