Burna Boy Afunguka Kutokea Kwenye Album Ya Beyonce
Mwanamuziki kutoka pande za Nigeria, Burna Boy amefanya mahojiano na kipindi cha Breakfast Club amefunguka mengi kuhusu Album yake pamoja na kufanya kazi na Beyonce
Burna Boy alifunguka kuhusu kutokea kwenye album ya ‘The Lion King: The Gift” kuwa hafahamu ni jinsi gani alifikia hatua ya kufanya kazi na Beyonce kwasababu hakuwahi hata kukutana nae uso uso, tamko la kufanya ngoma na Beyonce lilitoka kwa mama yake mzazi ambaye ni meneja wake.
Burna Boy alisema kuwa hatumii sana mitandao ya Kijamii, alisema Application pekee ambayo ipo kwenye simu yake ni “Whats App’ hapendi mitandao ya kijamii kutokana na watu wengi kufuatilia vitu vya watu wengine na pengine watu wangekua wanafatilia mambo yao basi Dunia ingekua kwenye sehemu nzuri na aliongezea na kusema hapendi kuongelea kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na mwanadada Stefflon Don.