Cassper Nyovest Anatamani Angekua Msanii Wa Nigeria.
RAPA kutoka South Africa, Cassper Nyovest ameamua kufunguka kuwa anatamani sana angekua msanii wa Nigeria.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Cassper Nyovest amefunguka wakati akimjibu shabiki wake aliyemwambia kuwa anatamani angekua anatoka nchini South Africa kwa kina Cassper, ila Cassper Nyovest alimjibu shabiki uyo “Kiukweli hata Mimi Natamani Kama ningekuwa natokea Nigeria, Upendo wanaouonesha kwa wasanii wao, Wanavyosherekea tamaduni zao, Asilimia 90 ya vitu wanavyovionesha na kuvipiga kwenye TV na Radio ni vya kwao, Wanasherekea muziki wao kila sehemu walipo duniani na wana umoja kwenye Muziki, Ndoto yangu”.
.
Toa Maoni Yako Hapa