Sambaza

Chemical aja na ‘Kagoma’, Azungumzia wanaume

MWANADADA anayetikisa katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’ ametambulisha ngoma yake mpya ya Kagoma huku akimwaga mauno kunogesha utambulisho huo.

Chemical aliyewahi kutamba na ngoma kibao kama Marry Marry na Asali akiwa na Beka Flavour alitambulisha ngoma hiyo ndani ya Bongo 255 kupitia +255 Global Radio inayoruka moja kwa moja kutokea mjengoni Global Group, Sinza Mori jijini Dar.

Mbali na kuitambulisha kwa mbwembwe ya kukata mauno,Chemical alisema video ya ngoma hiyo inayosubiriwa kwa hamuinatarajiwa kutoka Ijumaa hii ikiwa chini ya Dairekta Chriss.

“Kwanza nina mpango wa kuja na EP yangu (Extended Playlist au Albamu ya ngongeza) ambayo itakuwa na ngoma zangu kadhaa,” alisema Chemical.

Pia mkali huyo wa michano alizungumzia kuandika ngoma maalum kwa ajili ya marehemu Ngwair huku akisema kuwa aliyekuwa mkali mwingine marehemu Godzilla aliwahi kumsaidia sana katika muziki wake.

Akigusia suala la Mahusiano, Chemical amesema kuwa anatamani mwanaume wake awe ni ‘Mgumu’ ili aweze kumtii na kumheshimu, na sio wanaume Mabishoo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey