Shahidi Wa kesi Ya A$AP Rocky Amekamatwa Kwa Kesi Ya Wizi
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa kesi ya Rapa A$AP Rocky imeanzwa kusikilizwa jana Julai 30 mwaka huu katika mahakama iliyopo mjini Stockholm nchini Sweden.
A$AP Rocky kwa sasa bado anasota rumande amekanusha mashtaka dhidi yake, wakili wake ameieleza mahaka kuwa hakusababisha majeraha kwa makusudi bali alifanya hivyo kwa nia ya kujihami baada ya kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Mustafa Jafari ambaye ndio mshataki kutaka kumfanyia vurugu.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa shahidi ambaye alitakiwa kutoa taarifa mbele ya Mahakama kuhusu kesi inayomuandama A$AP Rocky amekamatwa kwa kesi ya wizi na ukabaji huku Mustafa Jafari ambaye anadai kushambuliwa na A$AP aliwahi kushtakiwa kwa kosa la kumpiga mtu kwenye mtaa wa Stockholm mwaka 2016.
Toa Maoni Yako Hapa