Sambaza

Vanessa Mdee ‘Amvaa’ Cyril Kamikaze na Maneno Makali

Malkia wa Bongo Fleva kwa sasa, Vanessa Mdee ameonyesha kuchukizwa na kauli Cyrill Kamikaze ambaye alikuwa shemeji yake kwa Jux, ambayo imepelekea Vanessa kumtolea maneno makali bila kuficha.

Kamikaze aliwahi kusema kwa sasa akiambiwa achague kati ya Vanessa Mdee na Mpenzi mpya wa Jux aitwaye Nnayika, atamchagua Nnayika kwa sababu rafiki yake ndio yupo nae kwa sasa na wala hawezi kumpinga Jux kwenye uamuzi wake, maneno ambayo yamemkera Vanessa na kuamua kufunguka.

Wawili hao kwa sasa wamekuwa hawana mawasiliano mazuri baada ya kuvunjika kwa penzi la Jux na Vanessa, ambapo hadi sasa kila mtu amemu-unfollow mwenzake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Akipiga story na kituo kimoja cha Radio nchini, Vanessa Mdee amesema sababu za kumu-unfollow Cyrill Kamikaze kwenye mtandao huo ni kutokana na maneno ambayo aliyaandika katika moja ya post zake baada ya kuachana na Jux, ambayo hakuyapenda.

“Kuna kitu alipost alinikera, sipendi mwanaume ambaye anatabia za kike Kuna post na maneno alikuwa anazungumza sikuyapenda kwahiyo nikamu-unfollow”.  Amesema Vanessa.

Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa hivi sasa yuko single na aliwahi kukiri kuwa kuvunjika kwa mahusiano yake na Jux kumemuumiza hasa baada ya Jux kuanza kumuanika katika mitandao ya kijamii mpenzi wake mpya.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey