Sambaza

Beka Ibrozama: Ruge Alinibadilisha Kimuziki

MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kutikisa na Ngoma ya Natumaini, Beka Ibrozama amesema hakuna kitu ambacho hatakisahau katika maisha yake kama kubadilishwa kimuziki na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

Akizungumza na +255 Global Radio kupitia Bongo 255, Beka aliyewahi pia kuwa katika Jumba la Kuibua Vipaji la THT alisema kuwa, Ruge alimsaidia sana lakini ilifika kipindi akaomba kuondoka na kuruhusiwa.

“Nilitoka THT nikamwambia Ruge naomba niondoke akasema sawa umeona nenda lakini hapa (THT) ni kama nyumbani, nilivyotoka nikawa sipo chini yake nikaingia katika uongozi mwingine ambao hawakujipanga vizuri nikawa kimya.

“Mara ya mwisho nilikutana naye tena wakati naachia wimbo wangu wa Kangaroo akaniambia unachokifanya Beka ni kizuri lakini ugali ni chakula nalo pilau ni chakula lakini usije kupeleka ugali kwenye harusi nikamuuliza unamaanisha nini akasema fikiria tu. Baada ya kupita kipindi ndiyo nikaelewa naimba sana lakini gemu la sasa halitaki hivyo,” alisema Beka anayetikisa kwa sasa na Ngoma ya Mbio.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey