Sambaza

Pamoja Sanaa Group Kurejea kwa Kasi ya Ajabu

Pamoja Sanaa Group ni moja ya kikundi cha sanaa chenye lengo la kukuza vipaji vya uigizaji hapa nchini.

Agosti Mosi, 2019 kikundi hiki kimetembelea Ofisi za Global Goup zilizopo Sinza Mori jijini Dar es salaam kujionea utendaji wa kazi namna ulivyo katika ofisi hizo.

Wakizungumza viongozi wa kundi hilo kwenye kipindi cha Radio +255 Global Radio walisema kuwa kikundi chao kimeanzishwa mwaka 2013 kikiwa na lengo la kukuza vipaji vya wasanii wa maigizo huku kikiwa na lengo la kuielimisha jamii kupitia maigizo.

Aidha viongozi walifafanua kuwa kikundi kimejikita katika uzalishaji wa Filamu pamoja na Tamthilia ambazo tayari baadhi wamesha zitengeneza na kuruka kupitia mitandao ya kijamii.

Kikundi hicho kilibainisha kuwa kilisitisha kutoa kazi zake za kisanaa na kupeleka sokoni kutokana na kuyumba kwa soko la Filamu Nchini kikihofia kupata hasara kutokana na mauzo hafifu.

Aidha kimesema kinaweka mambo sawa ili kiweze kurejea na kasi kubwa katika soko la filamu kwa ushindani wa hali ya juu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey