Sambaza

Q Chillah : Gharama za Video zangu Unajenga Nyumba

Msanii nguli katika ‘Industry’ ya Bongofleva Abubakar Shabaan Katwila almaarufu kama Q Chillah, leo Augosti 2, 2019 amefanya mahojiano maalumu na + 255 Global Radio katika kipindi cha Bongo255.

Q Chillah ambaye ‘ameshikwa mkono’ na Harmonize siku za hivi karibuni kwa ajili ya kumrudisha kwenye sanaa ya muziki, mbali na kuja kutambulisha nyimbo zake mpya alizotoa ambazo ni My Boo (Remix), Nionyeshe na Go Low ambazo zote ameshirikiana na Msanii Harmonize, pia amezungumzia maisha yake, alivyoyumba kimuziki na changamoto alizopitia yeye na familia yake baada ya anguko lake la kimuziki.

” Watoto wangu wamesoma kwa manyanyaso sana kwa sababu ya mapito ya mimi baba yao. Lakini nashukuru mungu nimepata nafasi nyingine na ninajua wapi nilikosea.”

Akizungumzia kuhusu gharama ya video zake zilizotoka hivi karibuni, Q Chillah amesema video hizo zimegharimu pesa nyingi sana ambazo ni zaidi ya Milioni 40, gharama ambayo yote ametoa msanii Harmonize. Akaongeza kuwa Harmonize ni mdogo kiumri, lakini anamuongoza kwenye mambo mengi sana kisanaa na amemuhakikishia kuwa baada ya miezi michache ataanza kupiga show za zaidi ya Milioni 20.

Alipoulizwa kuhusu kumsaidia Chid Benz aachane na matumizi ya madawa, Q Chillah amesema ” Chid Benz ni msanii mkali sana kwa hapa Afrika Mashariki, nampenda sana. Anahitaji msaada wa ziada kurudi kwenye mstari sahihi, nikiweza nitamsaidia.” Ameongeza Q Chief huku akimpa ushauri huo huo Msanii mwenzie TID kuwa aachane na tabia aliyonayo, na arudi kwenye tasnia.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey