Sambaza

Diamond Afunguka, Kuwa na Mahusiano na Lulu Diva

Msanii Diamond Platnumz amekanusha vikali tetesi za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Lulu Abbas aka Lulu Diva. Tetesi hizo zilianza kusambaa baada ya video kusambaa mitandaoni zikimuonyesha Diamond Platnumz akiwa ‘Close’ na msanii huyo ‘sexylady’ wa Bongofleva katika party uzinduzi wa Album ya RJ the DJ iliyofanyika Mlimani City.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, Diamond Platnumz aliamua kwenda kujibu Hoja hiyo kupitia comment kwenye Ukurasa mmoja wa Instagram uliokuwa umechapisha habari kuhusu tetesi hizo ;

Baada ya kuchapisha maoni yake kuhusu tetesi hizo, dada yake Esma Platnumz pia amemuunga mkono kwa kitendo alichokifanya cha kukanusha tetesi hizo hadharani na kuandika ” Bora maana wao wanawaza kubomoa familia za wenzao kwa Us**** wao, Mfyuu “

Kwa upande wa Lulu Diva, naye ameonyesha kukerwa na tetesi hizo na kuamua kujibu comment ya moja ya mashabiki wake katika ukurasa wake wa Instagram.

Hii sio mara ya kwanza kwa Msanii Diamond Platnumz kuhusishwa kutoka kimapenzi na baadhi ya warembo nchini licha ya kuwa katika mahusiano.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey