Sambaza

Jux Afunguka Sababu Iliyomfanya ‘Amteme’ Vanessa

Msanii Juma Jux amefunguka chanzo cha ugomvi uliopelekea kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi, Vanessa Mdee. Akipiga story na moja ya Televisheni ya mtandaoni hapa Tanzania, Jux ameeleza kuumizwa na kitendo alichokifanya, ambacho ndicho kilipelekea penzi lao ‘kuvunjika’.

“Chanzo cha ugomvi ni picha aliyopiga Vanessa na Ice Prince, alipiga picha ambayo sikuipenda na akaipost instragram “  Amesema Jux.

Akaongeza kufafanua kuwa

” Nilikuwa nimesafiri, mara nikaona amepost picha Instagram akiwa na Ice Prince. Nilikuwa embarrassed kwa sababu nilikuwa nipo na marafiki zangu, nilijua ni kazi na nikaamua kupotezea lakini ndani sikujisikia vizuri, Vee akaniambia kama sijapenda basi aifute….Mie nikamwambia aachane na mimi atafute mwanaume mwingine, ilikuwa ni utani lakini mwenzangu alichukulia serious na ndio mpaka leo tuko hivi. Ninajutia ile kauli yangu sana na kiukweli sikupaswa kusema vile.”

Kwa upande wa Vanessa Mdee, alishawahi kukaririwa akisema kuwa ameumizwa na kitendo cha Jux kumpost girlfriend wake mpya  kwenye Mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey