Sambaza

R Kelly Kufungwa Miaka 195 Jela

Msanii nguli duniani wa Miondoko ya R N B,  R. Kelly anayekabiliwa na mshitaka 13 ya unyanyasaji wa kingono huenda akafungwa Miaka 195 endapo atapatikana na hatia.  R . Kelly anatarajia kupandishwa kizimbani tena tarehe 14, Septemba 2019 baada ya siku ya jana kusomewa mashitaka hayo 13, yakiwemo kunyanyasa, kudhalilisha, na kushambulia wanawake kingono pamoja na kuwarekodi watoto wadogo picha zisizokuwa na maadili.

Baada ya kupandishwa kizimbani hapo jana Shirikisho la Mahakama na waendesha mashtaka wa kesi hiyo, wamesema R.Kelly atarudishwa tena mahakamani Septemba 14, kama akikutwa na hatia atapata adhabu ya kifungo cha miaka 195 jela.

R.Kelly kwa sasa amerudishwa mahabusu na wanasheria wake wamesema mteja wao amenyimwa haki kutokana ya kutopewa dhamana.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey