Sambaza

Rihanna ‘Amtolea Uvivu’ Rais Donald Trump…

Msanii maarufu duniani Robyn Rihanna Fenty almaarufu kama Rihanna, ameamua kumtolea uvivu Rais wa Marekani na kufunguka mambo yaliyomkera hasa ndani ya kipindi hiki cha utawala wa Rais Donald Trump. Rihanna ameonyeshwa kukerwa na serikali ya Trump hasa baada serikali kukaa kimya kuhusu mashambulio ya kigaidi yaliyoua watu karibia 30 siku za hivi karibuni.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Rihanna amechapisha moja kati ya tweets alizoandika Rais Donald Trump kuhusiana na mashambulio ya kigaidi na kumshushia lawama nzito kwa kutokuchukua hatua yoyote juu ya mashambulio hayo;

yametokea matukio mawili ya kigaidi kwenye nchi yako, watu karibia 30 wasio na hatia wamepoteza maisha, sasa hivi imekuwa rahisi mtu kununua silaha kama AK-47  ili akafanye shambulio kuliko kupata Visa”.

Rihanna aliendelea kuandika kuwa Dunia inaifikiria Marekani ndio Nchi inayoonekana kufuga magaidi na majambazi kutokana matukio yaliyotokea wikiendi hii.

Siku ya Jumamosi na Jumapili watu 29 walifariki dunia kwa matukio tofauti ya kushambuliwa kwa risasi katika miji ya California na Texas, lakini hadi sasa Donad Trump hajachukua hatua yoyote zaidi ya kutoa pole kwenye mtandao wa Twitter.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey