Sambaza

Beyonce Kuirudisha Destiny’s Child kwa Kishindo

Kundi la Muziki la Destiny’s Child ambalo lilikuwa likiundwa na Beyonce Knowles, Michelle Williams pamoja na Kelly Rowland kabla ya kuvunjika mwaka 2006, liko mbioni kurudi kwa kasi baada ya kuwa ‘Inspired’ na kundi la Spice Girls.

Vyanzo vya karibu na wasanii hao wa Destiny’s Child ambao walifanya vizuri sana mwanzoni mwa miaka ya 2000 vinasema kuwa Beyonce , Michelle na Kelly wamekuwa wakikutana mara kwa mara kwa ajili ya kupanga ujio wao mpya hapo mwakani 2020, mwaka ambao pia watakuwa wanaadhimisha miaka 20 ya kundi lao.

” Beyonce amekuwa akijitahidi sana kulirudisha kundi hilo kwenye ramani ya muziki na muda mzuri anaoona unafaa ni mwaka 2020 kwa sababu ndio mwaka ambao kundi hilo litakuwa linaadhimisha miaka 20 toka lianzishwe ” Chanzo cha karibu na wasanii hao kimeliambia Gazeti la The Sun.

Kitu kilichomsukuma Beyonce kuanza kupanga kulirudisha kundi lao  upya ni baada ya kuona ujio mpya wa kundi la Spice Girls, kitu ambacho kimemfanya aanze kupanga kufanya makubwa zaidi yao. Mbali na kutoa album pia wamepanga kufanya tour kubwa Marekeni na Bara la Ulaya ambayo itakata kiu ya mashabiki wao waliokuwa wamewa ‘miss’ kwa muda mrefu.

Baada ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2006, Kila mmoja aliamua kufanya kazi kama ‘Solo’ na kuwa na mafanikio makubwa huku Beyonce akiwa kinara kwa kutoa album 6 toka kundi hilo livunjike, mojawapo ikiwa ni album ya ‘The Lion King’  ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey