Sambaza

Harmonize Kujiondoa WCB? Hiki Chaweza Kuthibitisha?

Moja kati ya story kutoka ‘Lebo’ ya WCB ambazo zinasambaa mtaani kwa kasi ni story ya Harmonize kujiengua katika lebo hiyo na kuanzisha Lebo yake.  Kwa nyakati tofauti Harmonize amekuwa akikanusha tetesi hizo na kuwataka waandishi wanaouliza sana kuhusu suala hilo waache kufocus kwenye ‘mambo negative’ na badala yake waangalie mambo yanayojenga zaidi.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, huku wahusika wakikanusha kwa zaidi ya mara moja, kuna mabadiliko ameyafanya Harmonize katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ni moja kati ya ishara ambazo zinaashiria kuwa Harmonize huenda akaachana na Lebo hiyo iliyo chini ya Msanii Diamond Platnumz.

Ukurasa wa Instagram wa Harmonize ukiwa na Hauna Maelezo ya ‘Signed Under WCB Label’

Kabla ya hizi tetesi kusambaa, Harmonize pamoja na wasanii wengine wote wa WCB walikuwa wakitumia ‘Description’ inayosomeka ‘ Signed Under WCB Lebel ‘, Kitu ambacho Harmonize amekiondoa kwenye Bio ya Ukurasa wake wa Instagram na Kuacha Hashtag ya #WCB4LIFE

Tazama Kurasa za wasanii wote walio chini ya Lebo ya WCB, tofautisha na Kurasa ya Harmonize

Ukurasa wa Instagram wa Queen Darleen ukiwa na Maelezo ‘Signed Under WCB Label’
Ukurasa wa Instagram wa Lava Lava ukiwa na Maelezo ‘Signed Under WCB Label’
Ukurasa wa Instagram wa Mbosso ukiwa na Maelezo ‘Signed Under WCB Label’
Ukurasa wa Instagram wa Rayvanny ukiwa na Maelezo ‘Signed Under WCB Label’

Siku za hivi karibuni Harmonize alitangaza kumrudisha Q Chillah kwenye ramani ya muziki na kusimamia kazi zake chini ya ‘Konde Gang’ hali iliyozua maswali mengi na kuwaaminisha watu kuwa inawezekana tetesi zinazosambaa mtaani ni za kweli.  Tayari Q Chillah ameshatoa kazi nne chini ya usimamizi wa Harmonize ambazo ni Nionyeshe, Pepeta , Go Low, My Boo Remix

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey