Sambaza

BREAKING NEWS! Lori la Mafuta Lalipuka, Laua Watu Moro

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, lori la mafuta limelipuka asubuhi hii Agosti 10, maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro na kuua idadi kubwa ya watu ambayo inakadiriwa kufikia zaidi ya watu 54.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa idadi kubwa ya watu aliofariki ni madereva wa bodaboda waliokuwa wakiiba mafuta katika Lori hilo lililopata ajali, na watu waliokuwa karibu wakishuhudia ajali hiyo.

Chanzo cha moto kinaelezwa kuwa ni kitendo cha mtu mmoja kuchomoa battery ya gari na kusababisha cheche ambazo ndizo zilisababisha moto kuripuka.

Bodaboda zikiwa zimeteketea kwa moto baada ya lori kulipuka.
Bodaboda zikiwa zimeteketea kwa moto baada ya lori kulipuka.
Baadhi ya watu waliofariki katika Ajali ya Lori la Mafuta
Askari Polisi wakiwa eneo la tukio, wakisaidia kuokoa Majeruhi na Watu waliofariki
Lori likiwa linateketea kwa Moto, Maeneo ya Msamvu Morogoro
Baadhi ya boda boda zilizoteketea kwa Moto katika ajali ya Lori lililoripuka Maeneo ya Msamvu, Morogoro
Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey