Rosa Ree Afungukia ‘Kupokonywa Nyumba na Gari’
‘Rap Goddess’ Rosa Ree amefunguka kuhusu kupokonywa gari na nyumba na management yake iliyokuwa ikimsimamia. Mwaka 2018 Rose Ree alipata dili nono baada ya kuingia mkataba na kampuni ya Dimo Production, kampuni ambayo ilikuwa ikisimamia kazi zake za muziki. Katika mkataba wake, Rosa Ree alipewa nyumba, gari pamoja na pesa zaidi ya shilingi milioni 400.
Akipiga story na kituo kimoja cha televisheni hapa Bongo, Rosa Ree amefafanua kuhusu kupokonywa nyumba na gari alilopewa alipokuwa akisimamiwa na kampuni hiyo, Rosa Ree amesema;
“Hakuna kitu kibaya kilichotokea ila kila kampuni ina sheria zake na mnapokuwa mna mkataba basi kuna kuwa na makubaliano, gari na nyumba zilikuwa ni mali ya kampuni zilibaki ofisini kwa sababu ni mali za ofisi, mimi niliendelea kuhangaika kivyangu namshukuru mungu hakuniacha kinyonge sasa hivi nimepata vya kwangu”.