Harmonize, Nandy Wawekewa ‘Kigingi’ USA
WASANII wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize na Nandy, wamekwama kusafiri kuelekea nchini Marekani kwenye Tamasha la One Africa Music Festival lililofanyika juzi usiku, Jumamosi, Agosti 10, 2019, nchini humo.
Harmonize na Nandy ni kati ya wasanii waliopaswa kutumbuiza kwenye tamasha hilo linalojumuisha wasanii mbalimbali kutoka Afrika akiwemo Wizkid kutoka Nigeria.
Kutoka Tanzania, Diamond pekee ndiye aliyefanikiwa kusafiri na kutumbuiza katika shoo hiyo, lakini Nandy na Harmonize walishindwa kutokana na kukosa VISA ya kuingia Marekani.
Harmonize ame-post kupitia Insta Story yake kwa kuandika VISA kisha akamalizia na emoj ya kulia. Kwa post hii wadau wa mambo wanadai VISA ndiyo iliyomkwamisha Harmonize.
Toa Maoni Yako Hapa