Bonsi Vibe Festival Yafunika Dar Live (Picha+Video)
Mwanamitindo, muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, akisalimia mashabiki kabla ya kutoa shoo usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
MASHABIKI wa burudani wa Bongo Fleva na Singeli, usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2019, katika kusherehekea Siku Kuu ya Idd walipata bonge la burudani kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar live katika Tamasha la Bonsi ambalo lilikuwa noma saaana aisee.
Wasanii ambao wametoa burudani ni mwanamitindo, muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, mtaalam wa Singeli Mzee wa Bwax, Easy Man na wakongwe wa Bongo Fleva, Chid Benz na Mr Blue wakisindikizwa na mkali wa kupuliza matarumbeta, Kiroboto OG .
Mpango mzima ulianza na matarumbeta ya Kiroboto OG kisha mkali wa singeli, Eazy Man, kupanda jukwaani naye kufuatiwa na mkali mwingine wa Singeli, Mzee wa Bwax, abapo alifunika ile mbaya.
Uhondo wa singeli ukiwa bado unasikiliziwa, mkali wa kuchana, Chid Benz, alivamia jukwaa na kufanya yake ambapo aliwateka mashabiki wa burudani waliokuwepo.

Hayo yakiendele,a Hamisa Mobeto naye alivamia jukwaa na kuanza makamuzi ambapo mashabiki waliofurika ukumbini hapo ilikuwa ni full shangwe. Aliyemaliza kazi ukumbini hapo ni Mr Blue ambaye alipiga shoo ya aina yake


