” Harmonize ana Tamaa ” Hatimaye Diamond Afunguka
Kwa muda sasa tetesi za Msanii Harmonize kuachana na Lebo ya WCB zimekuwa zikisambaa. Harmonize kwa upande wake amekuwa akigoma kulizungumzia suala hilo lakini dalili za kuachana na lebo hiyo amekuwa akizionyesha wazi, kama kufuta Maelezo kwenye Bio yake ya instagram yaliyokuwa yameandikwa ‘Signed Under WCB Label’ na kuamua kum-follow Alikiba msanii ambaye ni mpinzani mkuu wa Diamond Platnumz.
Baada ya giza hilo kutanda huku watu wengi wakiwa hawana Uhakika na kile kinachosambaa mitandaoni, Msanii Diamond Platnumz amechochea moto wa uvumi huo baada ya ku ‘twist’ mashairi ya wimbo wake ‘Baila’ na kutaja kuwa Harmonize ana tamaa, akiaminisha watu kuwa tetesi za Harmonize kuachana na Lebo hiyo ni za kweli.
” Siunajuwa wanamuziki vitabia vyao wamejawa tamaa, hasa wale kina Harmonize wamejawa tamaa.”
Diamond Platnumz amefanya tukio hilo hivi Karibuni alipokuwa akifanya Show zake nchini Marekani, mpaka sasa Harmonize hajajibu chochote kuhusiana na hilo.