Sambaza

Kipindi cha #Katambuga chazinduliwa Rasmi

Watangazaji wa Kipindi cha Katambuga Walivyopokelewa na Matarumbeta kwenye uzinduzi wa kipindi
... Mapokezi makubwa ya watangazaji wa kipindi cha Katambuga

MOJA Kati ya vipindi bora kabisa vya redioni hapa Tanzania, kipindi cha KATAMBUGA Kinachoruka hewani kupitia Radio ya mtandaoni nambari moja Tanzania +255 Global Radio kimezinduliwa rasmi leo katika ofisi za Makampuni ya Global zilizopo Sinza Mori, Dar es salaam.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (Jembe) akiongea jambo wakati wa Uzinduzi wa kipindi cha Katambuga

Katambuga ni kipindi  kilichojikita katika maudhui ya kijamii, matukio, maisha na hekaheka za mtaani, pia kinajihusisha na muziki na ngoma za uswahilini. Kwa kipindi kifupi toka kipindi hiki kianze kuruka hewani, kimepiga hatua kubwa kwa kuigusa jamii moja kwa moja kwa kuripoti matukio ya kijamii, kupatanisha watu pamoja na kusaidia kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji.

Mtangazaji wa Kipindi cha Katambuga, Aisha Hussein akiongea jamba katika hafla fupi ya uzinduzi wa kipindi cha Katambuga.

Wakizungumza katika sherehe fupi ya uzinduzi huo watangazaji wa kipindi cha Katambuga Aisha Hussein (Jike la Tembo), Zaliam Adam pamoja na Gabby Mtanzania wametoa shukrani zao kwa viongozi wa kampuni ya Global kwa kuwapa ushirikiano mkubwa, pia wasikilizaji wa kipindi chao na kuahidi kuendelea kufanya mambo makubwa yatakayowashangaza watanzania.

Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kipindi cha Katambuga

Naye mkurugenzi wa makampuni ya Global, Eric Shigongo ameeleza kuguswa na uwezo wa waendeshaji wa kipindi hicho na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwaahidi kuwapa ushirikiano mkubwa katika kutimiza malengo ya kipindi chao. Akiongea mbele ya wafanyakazi wa Global, Shigongo amewataka wafanyakazi kushirikiana kwa ukaribu na kusaidiana ili kila mmoja afanikiwe katika eneo analofanyia kazi.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kipindi cha Katambuga

Meneja mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho pia ametoa pongezi kwa watangazaji wa Katambuga na kusisitizia zaidi suala la kuthamini vipaji. “Nilikuwa siwafahamu baadhi ya watangazaji wa Katambuga, ila baada ya kukaa nao niligundua wana uwezo mkubwa sana na toka siku ya kwanza nimesikiliza kipindi chao, sijaacha kukisikiliza mpaka leo maana wana vitu tofauti kila siku” Aliongeza Mrisho.

Shangwe la uzinduzi wa Kipindi cha Katambuga, wafanyakazi wa Global wakipata burudani Kutoka kwa Kiroboto Matarumbeta
Keki kwa ajili ya uzinduzi wa kipindi cha Katambuga
Watangazaji wa Katambuga, Zaliam Adam (Kushoto) Aisha Hussein (Katikati) na Gabby Mtanzania wakikata Keki
Mkurugenzi wa Global, Eric Shigongo akilishwa keki na Aisha Hussein
Baadhi ya wasanii waliofika kushuhudia uzinduzi wa kipindi cha Katambuga, Ben Selengo (Kushoto), Mama Kanumba pamoja na Lumole Matovolwa
Watangazaji wa Katambuga wakiwa kwenye picha ya Pamoja na wageni waliotembelea Studio kushuhudia uzinduzi wa kipindi
Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey