Sambaza

Rais Ramaphosa wa Sauz Awasili Nchini

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na mkewe, Dkt. Tshepo Motsepe wamewasili nchini Tanzania na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo na kupokelewa na mwenyeji wao, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabundi ambaye alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli..

Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao utaanza keshokutwa Jumamosi, Agosti 17, 2019 jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey