Tweet ya Donald Trump kwa Miley Cyrus yawa Gumzo
Tweet aliyopost Donald Trump mwaka 2013 kuhusu kuvunjika kwa mahusiano ya Mwanamuziki Miley Cyrus na Liam Hemsworth imekuwa gumzo mitandaoni hasa baada ya Wanandoa hao kutengana tena kwa mara ya pili, mara ya kwanza couple hii ilivunjika mwaka 2013, Mwezi Septemba.
Baada ya Couple hii kutengana, tarehe 19, Septemba 2013 Donald Trump alitweet kuhusu ‘issue’ yao na kuandika. “@MileyCyrus – don’t worry about Liam. You can do much better and you have plenty of time—remain strong!” Akiwa anampa moyo Miley kuhusu Kutengana kwao, akaongeza kuwa anaweza kufanya makubwa zaidi, kinachotakiwa ni kuwa imara tu.
.@MileyCyrus – don’t worry about Liam. You can do much better and you have plenty of time—remain strong!
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) September 19, 2013
Tweet hii ya Rais Donald Trump imekuwa gumzo tena siku za hivi karibuni baada ya Mastaa hao kuachana tena.