Sambaza

‘Katambuga’ Yawaka Rasmi Global Radio (Picha +Video)

Watangazaji wa kipindi cha Uswahilini cha Katambuga (Kijiwe Dobo) wakipokelewa na wafanyakazi wa Global Group jana Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

JANA Agosti 16, 2019, kulifanyika uzinduzi rasmi wa Kipindi cha Uswahilini cha Katambuga (Kijiwe Dobo) kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa katika spika za +255 Global Radio.

Katambuga ni kipindi maalumu kinacholenga zaidi maisha ya Uswahilini, hasa ku?chua na kutatua matatizo na changamoto za jamii mbalimbali ambacho huruka kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku chini ya watangazaji mahiri, Odo Aisha (Kubwa la Maninja), Zari Baby na Gaby Mtanzania (Sauti ya Mwanaume).

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akishuhudia watangazaji wa kipindi cha Katambuga wakisaini kitabu cha wageni, ambao ni Odo Aisha (kulia ), Zari Baby (wa pili kulia) na Gaby Mtanzania (wa tatu).  Wengine ni  Meneja wa Vipindi Global Redio, Bori Mbaraka (wa pili kushoto)  na  Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (wa tatu kushoto nyuma).

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Mama Kanumba, Ben Selengo, Kiroboto OG ‘Mzee wa Matarumbeta’, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo na wafanyakazi wa makampuni hayo.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (Jembe) akiongea jambo wakati wa uzinduzi wa kipindi cha Katambuga. Kushoto ni Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, wengine ni Zari Baby (wa tatu kushoto), Odo Aisha  na Gaby Mtanzania.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, ndiye aliyeongoza shughuli hiyo ikiwemo sapraizi ya kuwapokea watangazaji wa hao wa  Katambuga na kuongoza zoezi zima la ukataji keki lililoambatana na uzinduzi wa kipindi hicho.

Odo Aisha (Kubwa la Maninja) akiongea.

“Tumeamua kufanya hiki kitu sisi kama uongozi tukishirikiana na hawa watangazaji wa Katambuga kwa kutambua uwezo na kazi yao kubwa wanayoifanya hasa ya kuisaidia jamii,” alisema Ally.

Zari Baby akisema jambo wakati wa hafla hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Katambuga,Odo Aisha alisema: “Tunaushukuru uongozi kwa kutambua uwezo wetu na kazi kubwa tunayofanya kwa kuwa tumekuwa sehemu ya kutatua matatizo ya jamii na tunaahidi kuongeza ubunifu zaidi.”

Gaby Mtanzania (Sauti ya Mwanaume) akitoa ujumbe kwa wafanyakazi wenzake.

Naye Shigongo ambaye alizungumza mambo mengi yenye mafundisho, alisema: “Endeleeni kufanya hicho mnachokifanya na sisi kama uongozi tutawasaidia, msiogope kufanya jambo kwa hofu ya kushindwa huko mbele, jitumeni na muonyeshe vipaji vyenu ambavyo Mungu amewapa.”

Mama Kanumba (katikati), mwigizaji Lumole Matovolwa  (kushoto) wakiwa na Shigongo. Kwa nyuma ni wafanyakazi wa Global Group, Glory Massawe (kushoto) na Martha Mboma.

Ili kusikiliza ‘live’ matangazo ya +255 Global Radio, tembelea tovuti ya https:// globalradio.co.tz/ au pakua App ya +255 Global Radio katika Play Store kwa kuandika 255 Global Radio.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey