Sambaza

Harmonize ‘Kupindua’ Meza ya Diamond Platnumz

Diamond Platnumz amekuwa akiongoza kwa muda mrefu sana kama msanii ambaye nyimbo zake zinatazamwa sana katika mitandao mbalimbali, hususan youtube. Rekodi aliyoiweka na video yake ya Nana, aliyomshirikisha Mr. Flavor ya kutazamwa zaidi ya mara Milioni 53 haijawahi kuvunjwa na msanii yoyote hapa Bongo.

Rekodi hiyo iliyowekwa na Diamond Platnumz inafukuziwa kwa kasi na msanii Harmonize ambaye ni msanii aliyekuzwa na Lebo ya WCB inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz. Harmonize kupitia wimbo wake wa ‘Kwangwaru’ aliomshirikisha Diamond Platnumz amefikisha views zaidi ya milioni 50, ikiwa ni tofauti ya views milioni 3 tu.

Kwa nyakati tofauti wadau muziki wamekuwa wakimtabiria makubwa msanii Harmonize kuwa atakuja ‘Kupindua’ rekodi iliyowekwa na Diamond Platnumz kimuziki kutokana na jitihada za kujikuza anazoonyesha kuzifanya.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey