Jay-Z Atuhumiwa Kwa Kuwasaliti Jamii Ya Watu Weusi
Mwanamuziki kutoka pande za Marekani Jay-z atuhumiwa kwa kuwasaliti jamii ya watu weusi huko nchini Marekani kwa kusaini mikataba ya kazi na NFL (NFL ni bodi ya Ligi ya Mchezo wa Mpira wa Miguu ambayo imekuwa ikihusishwa na ubaguzi wa wachezaji wenye asili ya Afrika)
Jay-z amefanya mahojiano na Kamishna wa NFL – Roger Goodell, mwandishi mmoja wa habari alimuuliza Jay kama ataendelea kupiga goti chini kushinikiza kupinga uonevu wa polisi dhidi ya watu weusi kama alivyoanzisha Kaep mwaka Jana? Jay-Z alijibu “Hapana, nafikiri tumeshamaliza kupiga goti na sasa kinachofata ni vitendo tu.”
Sasa basi mpenzi wa Colin Kaepernick alikuwa mtu wa kwanza kuanza kumkosoa mwanamuziki Jay-z na uamuzi wake, amemuita msaliti kwa kuungana na watu ambao walimfanya mpenzi wake (Colin Kaepernick) akose ajira mpaka sasa kwa kutetea haki za watu weusi tena kwa amani
“Umetumika kumzika Kaepernick ambaye wewe mwenyewe ulimuita ‘Icon’ wako.”