Sambaza

Lorraine Mariot, Miss Universe 2015 anayefanya Makubwa

Lorraine Mariot ambaye alikuwa mshindi wa Miss Universe Tanzania 2015, amefanya mahojiano maalum na +255 Global Radio na kuzungumzia mambo mengi kuhusiana na safari yake ya urembo na uanamitindo na kazi anazozifanya hivi sasa.

Baada ya kutwaa taji la Miss Universe Tanzania 2015, alienda kuiwakilisha Tanzania katika Shindano la Miss Universe la dunia na  baada ya hapo Lorraine aliingia rasmi kwenye biashara ya uanamitindo (Modelling) ambapo amefanikiwa kufanya kazi nyingi za ndani na za kimataifa pia. Kwa upande wa hapa Tanzania Lorraine amefanikiwa kufanya kazi na baadhi ya wasanii wakubwa akiwa kama video model, Juma Jux, Diamond Platnumz ft Linex kwenye video ya Salima. Pia amefanya video na Eddy Kenzo wa Uganda pamoja na wasanii wengine wa nje.

Ukiachana na kufanya video modelling na wasanii wakubwa, pia anajihusisha na fashion modelling, commercial modelling ambayo anafanya na makampuni mbalimbali ya matangazo hapa Tanzania na nje ya nchi.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey