Sambaza

Bob Junior Arudi kwa Kishindo, Aachia Mbili kwa Mpigo

 

Msanii Bob Junior akiwa ndani ya Studio za +255 Global Radio

MSANII Bob Junior ambaye alifanya vizuri sana katikati ya miaka ya 2000 kwa kuachia hit songs kama Oyoyo, Nichum na zingine nyingi  amefanya Exclusive Interview na +255 Global Radio katika kipindi cha Bongo 255. Mbali na kufanya utambulisho wa ngoma zake mbili ‘Katoto ka Kufinya’ na ‘Mpasuo’, Bob Junior pia amezungumzia Kuhusu kupotea kwake kwenye ‘Game’ ya muziki wa muda mrefu.

Msanii Bob Junior akiwa na Mtangazaji Sechelela Mazanda wa Bongo 255

Akizungumzia kupotea kwake kwenye game ya muziki, Bob Junior amesema kuwa alikuwa kimya kwenye muziki kwa sababu aliamua kurudi shule kujiendeleza kielimu.  ” Ukimya wangu ulitokana na Mosomo, wazazi wangu hawakutaka nifanye Muziki bila Elimu, Wakati nasoma nimeandika zaidi ya nyimbo 60. Na elimu yangu nimesomea Finland Masuala ya Telecommunication.. “

….. Bob Junior Akiwa ndani ya Studio za +255 Global Radio

Kuhusu Mahusiano yake na Diamond Platnumz, Bob Junior ameeleza kuwa wana mahusiano mazuri na wameshafanya ‘Project’ ya pamoja ambayo itatoka mwezi wa 12, 2019.  ” Mimi na Diamond Platnumz tulisaidiana Sana Ndio Maana wote tupo hapa na tunajulikana, na hakuna beef lolote kati yetu, tunaelewana sana na kuthibitisha hilo kuna ngoma ambayo tumefanya pamoja ambayo tutaiachia mwezi wa 12 mwaka huu..” Ameeleza Bob Junior.

Tazama Interview nzima ya Bob Junior hapa chini

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey