Sambaza

Hamisa Akumbushia ‘Ishu’ ya Kukataliwa na Diamond

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi hapa bongo ambaye pia ni mwanamitindo, Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu mahusiano yake na Diamond Platnumz yalivyo hivi sasa. Hamisa na Diamond wana mtoto mmoja (Daylan ) ambaye kipindi cha ujauzito wake, Diamond alimkana hadharani katika interview moja na kusema yeye sio baba wa mtoto huyo na kama baba wa mtoto anamsikiliza basi ajitokeze.

Akipiga story na moja ya televisheni moja ya mtandaoni, Hamisa amegusia kuhusu drama hizo na kukiri kuwa zilimuumiza sana lakini hivi sasa ameshasamehe na kuendelea na maisha kama kawaida, na kuwa mahusiano yake na Diamond Platnumz hivi sasa yako vizuri kwani walishasameheana.

” Nimepitia changamoto nyingi sana kwenye mahusiano na nimejifunza mambo mengi sana kupitia mahusiano yangu, unaweza kumpenda mtu na yeye akaonyesha kuwa anakupenda lakini ukweli unakuta ni kuwa hakupendi the same  way kama wewe unavyompenda. Na sio kila mtu unayekuwa naye anaweza kuwa Ex wako na huwezi kujua kuwa mtu atakayekuja kwenye maisha yako anaweza kuwa bora kushinda aliyepita…So sioni kama kuna haja ya kuwa na kinyongo naye ” 

Hamisa ameongeza kuwa hivi sasa Diamond Platnumz anaplay part kubwa sana katika maisha ya mtoto wake Daylan. ” Daylan anajua na anapenda sana kudance, na anamjua baba yake vizuri… huwa akiona video ya Diamond huwa anatulia anaangalia mpaka inaisha. Kuna vitu ambavyo wanafanana sana…”  Aliongeza Hamisa

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey