Sambaza

MwanaFa Afunguka Kuingia Kwenye Siasa, Ubondia

Msanii nguli wa HipHop na mfanyabiashara hapa nchini Tanzania Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa, amenyoosha maelezo juu ya watu wengi kulitaja  jina lake kama linaweza kuingia kwenye siasa.

Akipiga story na moja ya kituo cha radio nchini cha EA Radio, MwanaFa amesema “Sijui nini kinawafanya watu waamini kama naweza kuingia kwenye siasa, lakini huwezi jua zote ni kadari tu sijajua nilichopangiwa kufanya kesho. Naamini chochote nitakachoamua kufanya kitakuwa ni manufaa ambayo sio yangu tu ni kwa jamii nzima”.

Mwana Fa ameendelea kusema  kuwa hawezi kusema kama anaweza au hawezi kuingia kwenye siasa kwa sababu  suala hilo lipo katikati.

Licha ya kazi ya usanii na ufanyaji biashara Mwana Fa ni mjumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), pia ni mmoja wa watu maarufu ambao wana ushawishi mkubwa hapa Tanzania. Vilevile  Mwana Fa amesema bado anauwezo wa kucheza ngumi ulingoni na anaweza akapanda ulingoni kupambana kwa raundi zote 12.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey