Drake Ashtakiwa Kwa Kuiba Beat La Rapa Mwenzake
RAPA kutoka pande za Canada anaefanya kazi za muziki nchini marekani, Aubrey Drake Graham a.k.a Drake amefunguliwa Shtaka la kuiba mdundo wa muziki (beat) wa msanii mwenzake na kuutumia kwenye ngoma yake ya “In My Feelings”.
Mtandao wa TMZ umemtafuta msanii Samuel Nicholas III ambaye anamtuhumu Rapa Drake kumuibia kila kitu kutoka kwenye ngoma ya “Roll Call” ambao aliuachia mwaka 2000. Msanii huyo amewafugulia mashtaka Drake pamoja Republic Records, Asylum Records na Cash Money.
Toa Maoni Yako Hapa