Majirani Wasimamisha Ujenzi Wa Nyumba Za Kanye West
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa majirani wamemuitia polisi rapa Kanye West hii ni baada kelele kuzidi kwenye mradi wake wa ujezi wa nyumba zake kwa ajili ya kupangisha wananchi wa hali ya chini kwa gharama nafuu mjini Calabasas.
Imeripotiwa kuwa jirani mmoja aliwapigia simu polisi wiki iliyopita na kuripoti kuwa Mtaani kwao kelele zimezidi kutoka na ujenzi wa nyumba za kanye West, Polisi waliwasili Jumamosi Saa 1:30 Usiku na kukuta ujenzi ukiendelea ndipo walipoamua kusimamisha ujenzi huo kutokana na Kanye West kutokuwa na kibali cha kufanya ujenzi wa kudumu katika eneo hilo, na mamlaka ya ardhi imeamua kumpa siku kadhaa kumaliza ujenzi huo.
Toa Maoni Yako Hapa