Sallam Sk Athibitisha Harmonize Kuachana na WCB
MENEJA wa ‘Lebo’ WCB Sallam Sk ameamua kuweka ukweli wazi kuhusiana na Sakata la msanii Harmonize kujiondoa WCB. Akifanya mahojiano na Wasafi FM, Sallam Sk amesema kuwa
Harmonize moyo wake haupo WCB ila kimakaratasi Harmonize bado yupo WCB, na ameshaandika barua ya kuvunja mkataba na WCB na kufuata taratibu zote za kisheria.
Ameyasema hayo Sallam Sk na kuongeza kuwa wanashukuru kwa uungwana aliouonyesha wa kufuata taratibu zote za kisheria kuhusu kuvunja mkataba wake, na wao kama menejimenti watakaa kujadili ombi lake.
Alipoulizwa kuhusiana na Kampuni ya Zoom Production ambayo inamilikiwa na Harmonize akiwa na ubia na Diamond Planumz, Sallam amesema kuwa
” Zoom iliundwa nje ya kampuni ya WCB na ni mali ya Harmonize na Diamond Platnumz, kwa hiyo itabaki kuwa hivyo, hawa watu hawajagombana na wataendelea kufanya kazi pamoja” Amesema Sallam Sk.
Kwa muda mrefu kulikuwa na tetesi kuhusu Harmonize kuachana na Lebo hiyo ya WCB lakini hakutaka kuliweka wazi, japokuwa ishara za yeye kujiondoa WCB alianza kuzionyesha mapema hasa baada ya kuanzisha ‘Lebo’ yake inayoitwa Konde Gang, na kufuta utambulisho wa ‘Signed Under WCB Label’ kwenye ukurasa wake wa Instagram.