G Nako Aeleza Sababu za Kumuweka Kikwete Miaka 3
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Kutoka kundi la WEUSI, G Nako ameeleza sababu za kukaa na ‘profile picture’ moja kwa zaidi ya miaka Mitatu bila kuibadilisha. G Nako ameweka picha akiwa ameshikana mkono na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika ukurasa wake wa Instagram picha ambayo imeitumia kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuibadilisha
Akiongea na kituo kimoja cha radio nchini G Nako amesema kuwa sababu ya kuiacha hiyo picha ni kutokana na kumkubali sana Rais Kikwete.
“Kwa sababu namkubali tu yule mzee na napenda awepo pale nafikiri ni mtu ambaye nimetokea kumuelewa na nimeshawahi kukutana naye mara mbili au mara tatu nikatokea kumuelewa na nafikiri anastahili kuwepo pale na napenda aendelee kukaa pale hadi nitakapoamua”.
Toa Maoni Yako Hapa