Ukinifanyia Ubaya Lazima Nilipize – MwanaFa Afunguka
Msanii amefunguka kuwa yeye ni miongoni mwa watu ambao wanapenda sana kulipiza kisasi hasa kwa watu ambao wamemkosea.
Mwana Fa amezungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha televisheni hapa Bongo na kuongeza kuwa kulipiza kisasi ni imani ya mtu.
“Huwa nawapanga watu kwenye makundi nikigundua tunaishi vizuri nakuweka juu kama hatuwezani nakufungia vioo. Siwezi ku-deal na mtu asiye na maarifa, pia kila visasi vyangu ni kwa watu walionikosea kama nipo katika nafasi nita-deal nao tu, ila wakati mwingine wanasema kisasi ni chakula kizuri kukiacha kwa muda, baadae nakuja kukukata kichwa”.
Aidha msanii huyo amezungumzia suala la kuweza na bahati katika maisha, ambapo amesema huwa anaamini katika kuweza kwa sababu ni kitu cha kudumu na mtu anatakiwa akifanye kwa uwezo, ufundi na ujuzi.