Sambaza

College Box Concert Ilivyotikisa Alpha Secondary

Meza kuu ilivyonekana ikiongozwa na Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo (wa pili kulia).LILE Tamasha kubwa kuliko yote nchini linalohusisha wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari na vyuo nchini, High Xcul & College Concert limetikisa katika Shule ya Sekondari Alpha iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo wanafunzi wa shule hiyo, walimu, wasanii, wahamishaji na watu wengine kibao.

Mmoja wa wanafunzi wa Sekondari ya Alpha akionyesha kipaji chake.Katika Tamasha hilo lililoandaliwa na Makampuni ya Global Group na kudhaminiwa na Global TV, +255 Global Radio, Global App, Global Publishers na Sayona Drinks, lilipambwa kwa burudani kutoka kwa wanafunzi hao ambao walipanda jukwaani kwa awamu kuonyesha vipaji vyao vikiwemo kuimba, kudansi, speech, kareti na michezo mingine kibao.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Alpha jijini Dar es Salaam wakifuatilia kilichokuwa kikiendela.

Baada ya kuonyesha vipaji vyao, wanafunzi hao mbao walishinda katika vipengele mbalimbali walitunukiwa vyeti na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo kama ishara ya kutambua vipaji vyao na kuwa sehemu ya ‘familia’ ya Global ambayo miaka yote tangu kuanzishwa kwake imekuwa mlezi namba moja wa vipaji mbalimbali vya vijana na kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Mmoja wa wanafunzi wa Alpha Sekondari mwenye kipaji cha kuimba akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa meza kuu.

Akizungumza wakati wa kutoa nasaha kwa wanafunzi hao, Shigongo aliwaasa wanafunzi hao ambao ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita kusoma kwa bidii ili baadaye waje kulisaidia taifa lao Tanzania huko mbeleni.

Mwanafunzi akipokea cheti kutoka kwa mhamasishaji Luvanda baada ya kuonesha ujuzi wake.

“Nimejifunza jambo katika maisha, ili ufanikiwe ni lazima kwanza uwe na tabia njema, tabia hiyo itajenga nidhamu. Lazima uwe na nidhamu kwa walimu wako, nidhamu kwa wazazi wako, jamii, marafiki na hata ukianzisha biashara au ukiajiriwa uwe na nidhamu ya matumizi ya pesa, hii itakusaidia kufanya matumizi sahihi ya pesa yako na mafanikio utayaona.

Mhamasishaji Luvanda akizungumza na wanafunzi wa Alpha Sekondari juu ya mbinu mbalimbali za kimasomo.

Aidha, Shigongo amewaasa wanafunzi hao kujituma katika masomo yao na vitu wanavyofanya, kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao, kufanya kazi kwa bidii na kumkumbuka Mungu kwa kila wanalofanya. Shiagongo pia amekabidhi vifaa vya michezo kwa wanafunzi hao ikiwemo mipira ya soka.

Furaha kutoka kwa wanafunzi zikitawala

Mbali na Shigongo, wengine waliotoa nasaha ni mhamasishaji chipukizi, Najma Paul, James Mwang’amba na wengine.

Mmoja wa wanafunzi wenye kipaji cha kuimba akionyesha ujuzi wake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Global TV na Global Radio, Abdallah Ng’anzi na Borry Mbarakah waliwaasa wanafunzi hao na watu wote waliofika ukumbini hapo kupakua Applications za Global App na 255 Global Radio ili wapate maudhui mazuri ya habari motomoto zinazopatikana kwenye applications hizo.

Mwanafunzi mwenye ujuzi wa kuimba akipokea cheti.

Kwa upande wa Global App ina habari za kitaifa na kimataifa, matukio, burudani, video za nyimbo zote mpya, magazeti yote ya Global Publishers Championi, Spoti Xtra, Uwazi, Ijumaa, Risasi, Betika, Amani na Ijumaa Wikienda kwa Tsh 300 tu, pia utatazama Global TV, Global Radio, kusoma na kusikiliza hadithi za Eric Shigongo na kusoma habari zinazowahusu wanafunzi.

….Wanafunzi wenye vipaji vya kuimba wakiendeleo kuonyesha ujuzi wao.

Na kwa upande wa Global Radio App, utasikiliza radio bora inayosikika kote ulimwenguni pamoja na kusoma habari zote za birudani kutoka kila pande ya dunia.

Vyeti vikiendelea kutolewa.

Mbali hao, pia walikuwepo wasanii kutoka MJ Records ambao walipata fursa ya kupanda jukwaani na kugonga nyimbo zao huku wakishea love na wanafunzi hao kwa kupiga nao pichaz.

Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group akizungumza na wanafunzi wa Alpha Sekondari kuhusiana na namna wanavyopaswa kuzingatia masomoa yao.

Msimu wa kwanza wa College Box ndiyo kwanza umefunguliwa rasmi leo Agosti 24, 2019, na Tamasha hili litazunguka nchi nzima na kupita katika shule na vyuo mbalimbali kuongea na wanafunzi na kuwapa mbinu mbalimbali za kufanikiwa katika maisha yao.

Shigongo akiendelea kuzungumza na wanafunzi hao.

Kauli mbiu ya College Box ni Safari Imeanza hivyo jiandae, huenda next ikawa ni shuleni kwako au chuoni kwako.

Picha na Denis Mtima | GPL.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey