Madonna Amtetea Miley Cyrus Kuhusu ‘Kuchepuka’
Msanii mkongwe wa Pop Madonna ameamua kumtetea Miley Cyrus kuhusuiana na sakata la kutokua mwaminifu kwenye ndoa yake na Liam Hemsworth kabla ya kutengana. Miley amekuwa akiandamwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo kitu ambacho yeye mwenyewe amekubali.
“Thank GOD!! You are human!” Madonna alicomment kwenye post ya Miley aliyoiweka Instagram akizungumzia tetesi za kusababisha ndoa yao kuvunjika kutokana na kutokuwa mwaminifu.
“A woman who has lived. No need to apologize!!” Aliongeza Madonna akimaanisha kuwa hakuna haja ya kuomba radhi kwani mwanadamu siku zote hukosea na ni kitu cha kawaida.
Hii ndio Post ya Miley ambayo watu maarufu wengi wamekuwa wakimpa moyo kutokana na ‘Skendo’ hiyo inayotrend kwa sasa.
View this post on Instagram