Meek Mill Amefutiwa Mashtaka Ya Kukutwa Na silaha
Rapa kutoka pande za Marekani, Robert Rihmeek Williams maarufu Meek Mill amefikishwa mahakani na amefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kukutwa na silaha pamoja na dawa za kulevya mwaka 2008.
Mtandao wa TMZ umeripoto kuwa rapa Meek Mill ametangaza nje ya mahaka kuwa kwa sasa yupo huru baada ya kukiri makosa yake ya kukutwa na silaha.
Meek Mill alipatiwaa nafasi ya kusikilizwa upya shauri lake katika mahakama ya mjini Pennsylvania nchini Marekani.
Toa Maoni Yako Hapa