Sambaza

Papii Aitaja ‘Starehe’ yake Baada ya Kutoka Jela

Msanii Papii Kocha ambaye ni mtoto wa mwanamuziki nguli nchini, Nguza Viking amefunguka kuhusu starehe anayoipenda hasa baada ya kutoka jela. Papii Kocha pamoja na baba yake, Nguza Viking walikuwa wamefungwa kifungo cha maisha kabla ya Rais John Pombe Magufuli kuwasamehe na kuwaachia huru..

Akizungumza na kituo kimoja cha radio nchini Papii ameeleza kuwa starehe yake kuu anayoipenda ni kuimba pekee;

nilikuwa nau-miss muziki napenda sana muziki, nilikuwa napata nafasi ya kuimba lakini nikiwa huku inapendeza zaidi, mimi sio mtu wa wanawake na sifagilii hizo drama nina mke wangu inatosha na starehe yangu kubwa
ni kuimba
”.

Pia amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumrudisha uraini na kusema anampenda na anamuomba Mungu ampe maisha marefu yeye pamoja na familia yake.

Pia Papii Kocha amesema amjipanga vya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri kwenye onesho la burudani ;a Rhumba Night linalotarajiwa kufanyika, Ijumaa ambapo wasanii wakubwa kutoka Kenya, akiwemo kutoka kundi la Sauti Soul wanatarajiwa kutumbuiza.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey