Ray C Angilia Sakata la Harmonize na Diamond
Msanii mkongwe wa kike nchini Tanzania, Ray C ameamua kufunguka kuhusu sakata la Harmonize na Diamond Platnumz kwa jicho la tofauti kabisa.
Ray C ambaye aliwahi kufanya vizuri sana kwenye game ya Bongofleva mwanzoni mwa miaka ya 2000 kabla ya kupotea kwenye game baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya amepost kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika;
“Nawaita Motherfuckin Mafiazzzz!????wanachokifanya sasa ni kikubwa mno kwa nchi yetu!Mkiwa na akili za kina Ndumilakuwili na kina Madenge pembeni na Kina Pimbi hamtaelewa kamwe!Ila mkiwa na akili zenu za kuzaliwa basi mtaelewa kuwa hawa wawili wanachokifanya ni kupeperusha bendera moja tu nayo.” Ameandika Ray C
Toa Maoni Yako Hapa