Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Kufanya Muziki
Mwanamuziki maarufu Duniani, Edward Christopher Sheeran maarufu kama Ed Sheeran ametangaza kuwa antaka kuchukua mapumziko baada ya kufanya muziki kwa muda mrefu.
Ed Sheeran ametoa kauli hiyo ya kuchukua mapumziko kwenye muziki na itakuwa ni miezi 18 alipokuwa anafanya hitimisho la ziara yake ya ‘Divide World Tour’ mjini Ipswich baada ya miaka miwili ya kuzunguka na ziara yake hiyo yenye mafanikio zaidi kwa muda wote .
Ed Sheeran alinukuliwa akisema “Nimependa uwepo wenu hapa na tumemaliza ziara yetu mjini Ipswich. Hili ni tamasha langu la mwisho kwa takribani miezi 18.”
Hii ni baada ya watu zaidi ya milioni 9 kuhudhuria kwenye tamasha lake la ‘Divide World Tour’ iliyoanza mwezi Machi mwaka 2017 ndani ya Siku 893 amezunguka mataifa 46 kwenye miji 175 na kufanya shows 260, Crew ya watu 268 na Kilometa 311,029 alizipiga na kuingiza kiasi cha Trilioni 1.9 za Kitanzania.