Sambaza

DC Sarah Msafiri na Mikakati ya Kigamboni | +255 Global Radio

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa pili kulia), akisalimiana na Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, wakati akipokelewa katika ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Mhariri Mtendaji wa magazeti la Global Publishers, Saleh Ally, na kushoto ni Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli.

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri amesema kuwa wilaya yake imejipanga kuhakikisha inatokomeza uhalifu na unyanyasaji wa kijinsia ambao umekuwa ukijitokeza katika maeneo mbalimbali ya Kigamboni ikiwemo tukio la mwanamke Naomi aliyeuawa na anayedaiwa kuwa mumewe kisha kuchomwa moto kwa magunia mawili ya mkaa.

 

…Akisaini kwenye kitabu cha wageni.

Msafiri amesema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano ya +255 Global Radio alipotembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema wanapoona matukio kama hayo au viashiria vya unyanyasaji kama huo.

 

…Akikabidhiwa gazeti la Ijumaa na Mhariri Paul Sifael; moja ya magazeti ambayo huchapishwa na Global Publishers

…Akikabidhiwa gazeti la Championi Jumamosi na  Mhariri Lucy Mgina.

Aidha, DC Msafiri amewataka wananchi kuyaendeleza maeneo waliyopewa na wilayani humo kwani wasipoyaendeleza ndani ya miaka mitatu yatataifishwa na kuwa mali ya Serikali.

…Akiwa ndani ya studio za +255 Global Radio.

…Akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Global Group, Eric Shigongo.

Baada ya kuwasili DC Sarah ameoneshwa vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya ofisi zetu ikiwemo kitengo cha Globalpublishers, kinachozalisha Magazeti, kitengo cha Global TV mwisho akamalizia kufanya mahojiano na kitengo cha Global Radio.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey