Sambaza

Msanii Dudubaya (Konki Master) Aamua ‘KUOKOKA’

Msanii Nguli wa Bongofleva Godfrey Tumaini maarufu kama DUDUBAYA ameamua Kuokoka, kitu ambacho kimewaacha watu wengi mdomo wazi. Dudubaya ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijulikana kwa tabia zake ‘Ubabe’, aliingia matatani na kuitwa polisi mapema mwaka huu baada ya kutoa maneno machafu kuhusu aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa CloudsMedia, Ruge Mutahaba wakati wa msiba wake.

Baadhi ya Matukio mengine aliyoyafanya Dudubaya ni tukio lake la kuwataja watu maarufu Tanzania ambao wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Ushoga), ishu ambayo ilihusisha Watangazaji maarufu, wanamuziki na hadi baadhi ya viongozi wa dini.

Taarifa za Msanii Dudubaya kuokoka zilianza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, huku yeye mwenyewe akipost na kuandika ” MZIGO MZITO NIMEUTUA……..SINA ADUI TENA….SINA MSHINDANI TENA…BAADA YA KUSAMEHE YOTE NIMEYASAHAU……I AM KONKI 3 MASTER????”. Baada ya post hiyo pia aliweka video ikimuonyesha akiombewa na Mchungaji Boniface Mwambosa.

Baada ya kuweka post hiyo na habari kusambaa mitandaoni kuhusu tukio hilo, baadhi ya watu wamezungumzia tukio hilo akiwemo Emmanuel Mbasha ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili. Mbasha aliandika;

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey