Sambaza

‘Ndege’ Aliyonunua Jaguar Yazua Gumzo

Msanii kutoka Kenya ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Starehe, Charles Njagua Kanyi maarufu kama Jaguar amezua gumzo mitandaoni baada ya kununua ndege ‘mbovu’ na kuipeleka nyumbani kwake. Jaguar alikuwa ni miongoni mwa wateja waliojitokeza katika mnada wa ndege mbovu zilizokuwa zikipigwa mnada na mamlaka ya anga ya nchinini Kenya (KAA). Baada ya kununua ndege hiyo ambayo ndio ilikuwa mbovu kushinda zote, Mbunge huyo aliipeleka nyumbani. 

Kabla ya kuanza kuifanyia marekebisho baadhi ya watu walijitokeza mitandaoni na kumtolea maneno ya kashfa kuwa amenunua scrap metal ‘chuma chakavu’ ambacho hataweza kukifanyia marekebisho yoyote, bila kujua lengo la Mbunge huyo kununua ndege hiyo lilikuwa ni lipi.

 

View this post on Instagram

 

….progress

A post shared by Hon. Jaguar (@jaguarkenya) on

Kupita kurasa yake ya Instagram, Jaguar amepost picha za ndege hiyo ikiwa inafanyiwa marekebisho ndani ya bustani ya nyumba yake na kuandika ……” Progress” akiwajulisha watu wanaomfatilia kwenye mitandao ya kijamii lengo lake la  kuinunua ndege hiyo… Mpaka sasa hakuna anayejua hasa lengo la msanii huyo kuinunua ndege hiyo lakini inasemekana ameinunua kwa ajili ya kuwa ‘Kivutio’ kwenye nyumba yake.

 

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey