Faiza Ally Atoa ya Moyoni Kuhusu Sugu Kuoa
FAIZA ALLY ambaye ni mzazi mwenza wa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameamua kufunguka kuhusu tukio la Sugu kufunga ndoa.
Faiza amezungumza ikiwa ni saa chache baada ya Mbunge Sugu kufunga ndoa na mkewe Happines Msonga, ambapo kupitia mtandao wake wa Instagram, amesema licha ya Sugu kuoa bado ana mapenzi na yeye.
“Kuna mtu anayenipenda sana alinipa ratiba nzima mwezi mmoja kabla ya ndoa na kabla ya hapo nilijua kama wataoana ila siku ya tukio ni siku ya tofauti, hata mwanzoni nilipotaka kufanya jambo nilijikuta nakosa hisia za kufanya kwa sababu sina tena majonzi juu ya baba Sasha.”, amesema Faiza.
“nikimwangalia baba Sasha na mke wake sioni mtu wa kuniliza na najiuliza nilikosea wapi, kwa sababu nilikuwa mpenzi bora, nilikuwa mama bora kwahiyo sijapata mwanaume tu wa kunielewa mimi. Anaoa lakini najua bado ananipenda mimi“.
Amezungumza hayo Faiza baada ya Mh. Sugu kufunga ndoa takatifu katika kanisa Katoliki la Ruanda Jijini Mbeya, jumamosi ya tarehe 31, August 2019. Ndoa ambayo ilihudhuriwa na wabunge wengi wa CHADEMA.