Kevin Hart Apata Ajali Mbaya ya Gari
MWIGIZAJI Kevin Hart wa Marekani na watu wengine wawili jana (Jumapili) walipata ajali ya gari huko Calabasas, California, ambapo yeye na dereva wake, Jared Black waliumia vibaya maeneo ya migongoni.
Ajali hiyo ilitokea katika Barabara Kuu ya Mulholland ambapo gari la Kevin, aina ya Plymouth Barracuda, lilitoka barabarani na kuingia kwenye mtaro na kuparamia ua wa magogo na hivyo sehemu ya juu ya gari kuharibika vibaya.
Wawili hao walikimbizwa hospitali, ikiwa ni baada ya Kevin kujinasua katika gari hilo na kwenda kupata matibabu katika makazi yake. Hart alilinunua gari hilo mwezi Juni mwaka huu akijizawadia kutimiza miaka 40 ya kuzaliwa kwake.
Katika posti yake kwenye mtandao wa Instagram, Jumamosi, aliandika kwamba alikuwa amefurahi kutosafiri kwenda popote wakati wa wikiendi ambapo aliandika:
“Being home makes me happy….enjoy your weekend people!!!! #LiveLoveLaugh.”
Toa Maoni Yako Hapa