Sambaza

50 Cent Amlinganisha Chris Brown na Michael Jackson

RAPA kutoka Marekani, Curtis Jackson III ‘50 Cent’ amesema kwa mtazamo wake, staa wa Muziki wa R&B na Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ ni mfalme wa Pop kuliko Michael Jackson.  Kupitia ukurasa wake wa Instagram, 50 Cent alimsifia Chris Brown kuwa amefanikiwa zaidi kwenye muziki katika kipindi kifupi.

50 Cent alisema, Chris Brown amekuwa msanii wa saba mwenye mauzo makubwa nchini Marekani. “Chris Brown ameuza nyimbo kwa zaidi ya milioni 69.5 hii ni Marekani na kumfanya kuwa msanii wa saba kwenye mauzo kwa muda wote. Pia ana jumla ya RIAA milioni 1000, kwa hiyo CB (Chris Brown) kwangu namuona ni mfalme kuliko MJ (Michael Jackson),” aliandika 50 Cent.

Kwa mujibu wa muziki nchini Marekani, RIAA ni Jumuiya ya Utoaji Tunu kwa Wanamuziki wa Marekani ambayo huangazia mauzo ya albamu na nyimbo moja moja katika soko

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey