Brad Pitt Ajiunga na Kanisa la Kanye West
Rapa kutoka pande za Marekani Kanye West ameendelea kujipatia wafuasi wengi wa dini yake aliyoianzisha , na miongoni mwa wafuasi hao ni Ma-celebrities wakubwa duniani. Katika ibada ambayo huifanya kila jumapili, msanii huyo aliyetangaza kuachia album yake mpya ya nyimbo za Injili ‘Jesus is King’ amekuwa akijizolea wafuasi wengi kadri siku zinavyokwenda.
Jumapili ya tarehe 1, September 2019 Muigizaji maarrufu duniani Brad Pitt alikuwa na mmoja wa watu maarufu waliohudhuria ibada ya Kanye West ambayo hufanyika eneo la Watts, Los Angeles.
Rapa huyo ambaye haishiwi vituko wiki mbili zilizopita alifanyia ibada ya jumapili katikati ya barabara, kitendo ambacho kilizua gumzo duniani.
Toa Maoni Yako Hapa